Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 18 Aprili, 2018

Kylian Mbappe
Nyota wa PSG, Kylian Mbappe na Thiago Alcantara wa Bayern Munich ndio vinara kwenye orodha ya meneja wa Manchester City, Pep Guardiola kwenye usajili wa majira ya joto.

Meneja wa klabu ya Leceister City, Claude Puel amesema kuwa Harry Miguel hauzwi.

Zinedine Zidane anasisitiza kuwa hakuna tatizo lolote kati yake na straika wa klabu hiyo, Gareth Bale licha ya kumtoa nje wakati wa mapumziko kwenye mechi yao dhidi ya Juventus.

Kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches anayeichezea Swansea kwa mkopo amerejea kikosini akitokea majeruhi.
 
Tottenham inatakiwa kuwekeza fedha za kutosha kama itataka kushindana na Manchester City msimu ujao, kwa mujibu wa Ian Wright. (Sky Sports)

Hatima ya Edison Cavani katika klabu ya PSG iko shakani kufuatia ugomvi wake na Neymar kuendelea kugonga vichwa vya habari hadi sasa. (Le10Sport)
 
Antony Martial na Alvaro Morata ni vinara kwenye orodha ya washambuliaji watakaolengwa na Juventus kwenye usajili wa majira ya joto.

Juventus wamechoshwa na kusubiria uamuzi wa kiungo kutoka Liverpool, Emre Can na sasa wameanza kuandaa orodha ya wachezaji wengine, akiwemo Aaron Ramsey, Adrien Rabiot na Lorenzo Pellegrini. (Tuttosport

Mohamed Salah
Mohamed Salah anajenga Hospitali na Shule katika mji wa Nagrig nchini Misri, ambako ndiko alizaliwa kufuatia kuwa na msimu mzuri katika Liverpool.

Kiungo anayewaniwa na klabu ya Real Madrid, Paul Pogba anatarajiwa kusalia Manchester United licha ya kuwa na uhusiano mbaya na Jose Mourinho.

Uingereza itakuwa na mashabiki wachache kwenye Kombe la Dunia kwenye majira ya joto kuliko Peru na China baada ya uhusiano wao na Urusi kufika pabaya.

Leicester imeziambia Manchester United, Arsenal na Tottenham kutoa pauni milioni 50 kumnasa Harry Maguire.

Southampton inamtamani golikipa wa klabu ya Sheffield Wednesday, Keiren Westwood achukue nafasi ya Fraser Forster kwenye majira ya joto. (Sun)

Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola ameipa ofa klabu ya Paris Saint-Germain kumsajili mteja wake, huku Man Utd ikiwa tayari kumuuza Mfaransa huyo.

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City, Saido Berahino amechafua jina lake kwa kujikuta kwenye hatia ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara. (Daily Mail)

Manchester United 'wanategemewa' kumsajili beki wa klabu ya Valencia, Joao Cancelo, huku Matteo Darmian akiwa njiani kuelekea Juventus.

Jean Michael Seri
Chelsea wanapanga kumnasa nyota wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri kwa dau la pauni milioni 35 kwenye majira ya joto.

Liverpool bado haijakata tamaa ya kumsajili kiungo wa Napoli, Piotr Zieliński anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 57, baada ya kushindwa kumnasa nyota huyo miaka miwili iliyopita.

Arsenal ndio klabu pekee katika Ligi Kuu ya Uingereza inayopewa nafasi kubwa ya kuweza kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial.

Uongozi wa Stoke City unataka, Paul Lambert aendelee kuwa meneja wao hata kama klabu hiyo itashuka daraja. (Daily Mail)

Manchester City, Tottenham na Arsenal zinashindana kuipata saini ya straika wa klabu ya Norwich, James Maddison kwenye majira ya kiangazi. (Telegraph)

Kiungo wa klabu ya Newcastle, Jonjo Shelvey yuko mbioni kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia.

Juventus imemfanya mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial kuwa chaguo lao la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto. (Times)

Thomas Tuchel anakaribia kuteuliwa kuwa meneja mpya wa Paris Saint-Germain msimu ujao. (Guardian)

Daniele Rugani 
Beki wa kati wa klabu ya Juventus, Daniele Rugani anaripotiwa kuwa kwenye rada za Arsenal. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 18 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 18 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/18/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.