Loading...

Chelsea wamefikia makubaliano na Arsenal juu ya ada ya uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain


Kwa mujibu wa ripoti ya SkySports, Chelsea wamekubali kulipa kiasi cha fedha ambacho Arsenal wanakihitaji ili kumwachia nyota wao na wa timu ya taifa ya Uingereza, Alex Oxlade-Chamberlain.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 yuko 'St George's Park' pamoja na kikosi cha timu yake ya taifa ya Uingereza na tayari Sky Sports wanaeleza kwamba anaweza kufanyiwa vipimo vya afya katika sehemu maalumu ya mazoezi ya timu hiyo.

Mkataba wa Oxlade-Chamberlain na Arsenal utaisha mwishoni mwa msimu huu, pamoja na ule wa Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Kama ilivyo kwa Sanchez na Ozil, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa akisistiza kwamba anataka Oxlade-Chamberlain aendelee kuitumikia Arsenal kwa kipindi cha muda mrefu ujao.
Oxlade-Chamberlain alifanya mazungumzo na Wenger juu ya maisha yake yajayo Emirates kabla ya kuelekea mechi yao dhidi ya Liverpool, mazungumzo ambayo hayakuzaa matunda ingawa alipangwa kwenye kikosi cha kwanza kilichopoteza mchezo kwa kukubali kichapo cha goli 4-0 Anfield.

Oxlade-Chamberlain amekuwa akihusishwa na Liverpool pia, lakini inaonekana ameamua kusalia London na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Chelsea wamefikia makubaliano na Arsenal juu ya ada ya uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain Chelsea wamefikia makubaliano na Arsenal juu ya ada ya uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain Reviewed by Zero Degree on 8/29/2017 01:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.