Loading...

Chelsea wapewa hamasa ya kumsajili Alex Sandro


Chelsea wanatarajia kukamilisha usajili wa nyota wa Juventus, Alex Sandro katika majira haya ya joto.

Raia huyo wa Brazil (Alex Sandro) anatarajiwa kujiunga na Chelsea akitokea Juventus kwa paundi milioni 61 kiasi ambacho kinatarajiwa kuvunja rekodi ya ada ya uhamisho kwa klabu ya Juventus.

Mkurugenzi wa klabu ya Juventus, Beppe Marotta alikataa ofa ya kwanza ya paundi milioni 55.2 iliyotolewa na Chelsea. Hata hivyo, alimweleza nyota huyo kuwa endapo kiasi cha fedha watakachotoa kitakuwa kinachohitajika basi yeye hatakuwa na haja yoyote ya kumzuia kuondoka.

Mabingwa hao wa Italia watapata faida kubwa endapo watafanikiwa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliwagharimu kiasi cha paundi milioni 23 wakati anajiunga nao akitokea Porto.

Chelsea wamejipanga kuongeza ofa ikiwa ni pamoja na kujaribu kumpoza Antonio Conte ambaye anaonekana kutoridhishwa na jinsi mikakati ya usajili ilivyoenda mwanzoni mwa msimu tofauti na ambavyo matarajio yake yalikua.

Ada hiyo itavunja rekodi ya uhamisho 
ya paundi milioni 50 iliyolipwa kwa ajili ya uhamisho wa Fernando Torres kuja Chelsea mwaka 2011 na ile ya paundi milioni 47.5 iliyolipwa na Manchester City kwa Everton kumnasa John Stones mwaka jana.

Chelsea wanategemea kurejesha kiasi cha fedha watakachotumia 
kumsajili Sandro kwa kumuuza Nathan Ake kwenda Bournemouth kwa ada ya paundi milioni 20.
Chelsea wapewa hamasa ya kumsajili Alex Sandro Chelsea wapewa hamasa ya kumsajili Alex Sandro Reviewed by Zero Degree on 8/29/2017 12:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.