Loading...

Dawa ya wanaotapeli kwa kutumia simu za mkononi iko jikoni

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amewaonya watu wanaojihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi na kujitambulisha kuwa wao ni viongozi wa serikali kuacha mara moja, vinginevyo watakaobainika hatua kali zitachuliwa dhidi yao.

Alitoa onyo hilo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo ya kitapeli na kuwa baadhi ya watu wanaojihusisha na utapeli huo kutumia majina ya viongozi kusajilia simu zao ili kuwatishia watumishi.

“Vyombo vya dola vitakapowabaini watu hawa visiwachukulie hatua kimya kimya bali viwatangaze hadharani ili wawe mfano kwa wengine wenye tabia hizo,” alisema. 

“Nimepata malalamiko kuwa watu wamesajili hadi kwa jina langu na wanajitambulisha kuwa ni waziri wa mambo ya ndani, hivyo basi niwaombe watumishi kuacha kufanyia kazi maagizo yoyote ambayo yanatolewa na watu hao kwa njia ya simu na kujikuta wanatapeliwa fedha, ” alisema. 

Hata hivyo alisema kuwa watu wanaosajili simu ambao wamekuwa wakitumika kuwasajili watu ambao sio wenye majina halali, sheria itawabana.
Dawa ya wanaotapeli kwa kutumia simu za mkononi iko jikoni Dawa ya wanaotapeli kwa kutumia simu za mkononi iko jikoni Reviewed by Zero Degree on 8/17/2017 11:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.