Loading...

Grace Mugabe kufika mahakamani Afrika Kusini


Mke wa Rais wa Zimbabwe Grace Mugabe anatarajiwa kufika mahakamani nchini Afrika Kusini kufuatia madai ya kumshambulia mwanamke mmoja, kwa mujibu wa mkuu wa polisi nchini humo.

Fikile Mbalula, alisema kuwa Bi Mugabe hajakamatwa kwa sababu alitoa ushirikiano na kujisalimisha kwa polisi.

Alidaiwa kumshambulia mwanamke mmoja katika hoteli moja mjini Johannesburg.

Mwanamke huyo wa umri wa miaka 20 alidai kuwa Bi Mugabe 52, alimjeruhi usoni na kwenye kichwa na kuweka picha za majeraha kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi nchini Afrika Kusini walithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa ameandisha kesi ya kushambuliwa kwa minajili kumsababishia madhara makubwa ya mwili.

Sababu ya mwanamke huyo kushambuliwa katika 
shambulizi hilo linaloripotiwa kufanyika Jumapili jioni haijulikani.

Waziri wa habari nchini Zimbabwe Christopher Mushowe aliambia BBC kuwa hajafahamu madai hayo.

Bi Mugabe alikuwa nchini Afrika Kusini kutibiwa jeraha alilopata kufuatia ajali ya barabarani mwezi uliopita
Grace Mugabe kufika mahakamani Afrika Kusini Grace Mugabe kufika mahakamani Afrika Kusini Reviewed by Zero Degree on 8/15/2017 03:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.