Loading...

TFDA yateketeza tani 1.6 ya bidhaa feki Jijini Mwanza


Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), Kanda ya Ziwa imeteketeza tani 1.6 ya vyakula vya aina mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh2.8 milioni visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Mkaguzi Mwandamizi wa Chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa, Julius Panga amesema leo Jumanne, Agosti 15 kuwa bidhaa zilikamatwa wakati wa ukaguzi wa kushtukiza uliofanyika kwenye maduka ya bidhaa za chakula katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Amesema miongoni mwa bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na chumvi aina ya Kaysalt vifungashio vyake vinaonyesha ilitengenezwa kwa ajili ya soko la nchi jirani ya Kenya kwa kuandikwa.

“Inaonekana bidhaa hii iliingizwa nchini na kusambazwa kwenye maduka mbalimbali kinyume cha sura ya 219 ya sheria na kanuni ya uwekaji lebo kwenye vifungashio,” amesema Panga.

Bidhaa nyingine ni mafuta ya kupikia ambayo licha ya kuandikwa jina la ufuta kuonyesha yanatokanana mbegu ya ufuta, lakini uchunguzi umebaini yametengenezwa kwa malighafi ya mawese.

Panga amesema TFDA imelazimika kuyaondoa sokoni na kuyateketeza mafuta hayo baada ya walioingiza bidhaa hiyo kushindwa kutekeleza maelekezo ya kuwasiliana kufanya marekebisho ya jina kutoka ufuta kwenda mawese.

Bidhaa zingine zilizoteketezwa ni zilizoingizwa nchini bila kusajiliwa na zilivyomalizika muda wa matumizi.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, TFDA ilikamata na kuteketeza tani 63.7 za bidhaa mbalimbali za chakula zenye thamani ya Sh136.3 milioni katika mikoa ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Simiyu na Kagera.

Akizungumzia operesheni dhidi ya bidhaa feki na zilizoisha muda wa matumizi, Ramadhani Juma mkazi wa Nyamanoro jijini Mwanza aliomba zoezi hilo liwe endelevu kuokoa afya za walaji ambao wengi hawana ujuzi kubaini bidhaa zisizofaa kwa matumizi.

Makosa mengine yanayosababisha bidhaa kukamatwa na kuteketezwa huku wahusika wakitakiwa kulipia gharama ya uteketezaji ni kukosena kwa maelezo ya wazalishaji au watengenezaji pamoja na maelezo kuandikwa kwa lugha isiyoeleweka kwa walaji.

Wafanyabiashara au wazalishaji wanatatoa taarifa kwa hiari TFDA juu ya uwepo wa bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi hawatozwi gharama za kuteketeza bidhaa hizo.
TFDA yateketeza tani 1.6 ya bidhaa feki Jijini Mwanza TFDA yateketeza tani 1.6 ya bidhaa feki Jijini Mwanza Reviewed by Zero Degree on 8/15/2017 03:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.