Loading...

Iraq yatangaza mapumziko kwa wafanyakazi wote kufuatia ongezeko la joto


Waziri mku wa Iraq Haider al-Abadi ameamrisha wafanyakazi wote wa serikali kuchukua likizo leo Alhamis kutokana na kuwepo viwango vya juu zaidi vya joto.

Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia viwango vya joto kwenye mji mkuu Baghdad kufikia nyuzi 50C leo alasiri. 

Joto jingi pia linatarajiwa miji ya Basra na Mosul. Joto hilo jingi linaweza kusababisha ukosefu wa nguvu za umeme.

Viwango vya juu vya joto vinashuhudiwa kote eneo hilo na tayari vimeathiri maeneo ya bara Ulaya siku za hivi karibuni.

Wanasayansi wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha vifo vya watu 52,000 barani Ulaya mwaka 2100 ikiwa chocho hakitafanyika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Iraq yatangaza mapumziko kwa wafanyakazi wote kufuatia ongezeko la joto Iraq yatangaza mapumziko kwa wafanyakazi wote kufuatia ongezeko la joto Reviewed by Zero Degree on 8/10/2017 12:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.