Loading...

Kampuni ya Halotel kujenga minara mipya 47, kufikisha mawasiliano vijijini

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai, kabla ya kuanza kwa hafla ya kutiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu. Pamoja naokatika picha ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga.
Kampuni ya simu ya Halotel kwa kushirikiana na Serikali imetiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) tukio ambalo Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yoyote ya simu hapa nchini.

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akiwashuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga wakitia saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu
Kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko wa USCAF ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu yakifikiwa kwa haraka zaidi hivyo kwa hatua hiyo ya Halotel itawezesha huduma hiyo kufika maeneo hayo.

Lakini pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano hafifu.
Kampuni ya Halotel kujenga minara mipya 47, kufikisha mawasiliano vijijini Kampuni ya Halotel kujenga minara mipya 47, kufikisha mawasiliano vijijini Reviewed by Zero Degree on 8/19/2017 12:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.