Loading...

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akamatwa na Polisi


JESHI la Polisi mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa madai ya kuzidisha muda wakati akihutubia kwenye mkutano wake na wananchi jana Jumatano, Agosti 23, 2017 jijini humo.

Polisi wamedai kuwa Lema alimaliza mkutano wake saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kama ilivyo utaratibu.

Hivyo askari polisi walimzuia katika mzunguko wa barabara wa Mnara wa Saa (round about) kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari yake na kumuelekeza Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) mjini Arusha.

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili, endelea kufuatilia ukurasa wetu.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akamatwa na Polisi Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akamatwa na Polisi Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 12:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.