McGregor atalazimika kustaafu kutokana na kichapo atakachopata, Mayweather
Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 40 amepitwa uzito kwa kiasi kidogo na mpinzani wake Conor McGregor katika vipimo walivyofanyiwa wikendi iliyopita.
Lakini Mayweather hakuwa na shaka na suala hilo kama ambavyo bingwa huyo wa maasumbwi anaamini kwamba uzoefu wake mkubwa utamfanya atambe mbele ya McGregor.
Lakini Mayweather hakuwa na shaka na suala hilo kama ambavyo bingwa huyo wa maasumbwi anaamini kwamba uzoefu wake mkubwa utamfanya atambe mbele ya McGregor.
"Nimeshakutana na watu wa namna huyo kabla yake. Najua nini cha kufanya pale inapokuwa ni kwenye pambano kubwa kama hili," alisema Mayweather, ambaye alikuwa na uzito wa kilogram 67.8 na McGregor kuwa na kilogram 69.4.
"Uzito haukupi ushindi, bali ushindani ndio unaokupa ushindi."
Mayweather anaelekea pambano lake la 50 na yuko kwenye mapambano yake ya mwishoni kuelekea kustaafu, lakini anasisitiza kwamba, mpinzani wake pia atalazimika kustaafu masumbwi kufuatia kichapo atakachopewa.
"Haitakuwa kazi ngumu, utakumbuka baada nilimaanisha nini," alisema Mayweather.
"Hakika sina wasiwasi na uzito wake au vinginevyo, na hili litakuwa ndilo pambano la mwisho kwa Conor McGregor's pia.
"Mashabiki hawatapigana kwa ajili yako. Linakuwa ni swala linalowahusu watu wawili tu wanaokuwa ulingoni, usitegemee mashabiki.", alimalizia.
McGregor atalazimika kustaafu kutokana na kichapo atakachopata, Mayweather
Reviewed by Zero Degree
on
8/26/2017 03:58:00 PM
Rating: