Loading...

N'golo Kante amjibu Claude Makelele

Kiungo wa Chelsea, N'golo Kante amesema kuwa huwa anajisikia mwenye furaha kubwa mara zote anapopata ushauri kutoka kwa Claude Makelele.

Kante amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Conte tangu awasili Chelsea, akawa mchezaji wa kwanza kikombe cha Ligi kuu mara mbili mfululizo akiwa na klabu tofauti kufuatia ushindi wa taji hilo alioupata akiwa na Leicester na ule wa msimu uliopita akiwaa na Chelsea.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 pia alitunukiwa tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka, vile vile alitwaa tuzo ya FWA ya mchezaji bora wa mwaka baada ya kung'ara chini ya uongozi wa Antonio Conte kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu.

Lakini mwanzoni mwa mwaka, nyota wa zamani wa Chelsea, Claude Makelele alisema kuwa, Kante anatakiwa kuwa zaidi ya kiungozi ili achukuliwe kama 'mchezaji wa pekee'.

"Ambacho nampendea ni kwamba, ni mchezaji mkarimu sana," Makelele, ambaye aliitumikia Chelsea kwa miaka mitano na kushiriki mechi 71 na timu yake ya taifa, aliiambia 'SFR Sport'.

"Anacheza wakati uso wake ukitabasamu, na hicho ni kigezo cha kipekee. Ninatumaini ana uwezo mkubwa na nafasi ya kutosha kuliko mimi, lakini bado anahitaji kuonekana kama kiongozi."

"Simanishi awe nahodha wa klabu, lakini awe na muonekano wa kiuongozindani ya timu pale wenzake wanapomtazama tu, wafikirie kwamba “Tunaenda kupata ushindi” au pale anapowaeleza jambo, waondoke wakisema “Uko sahihi”.

"Atakapokuwa na haiba hiyo, atakuwa mchezaji wa kipekee. Hapo ni atakapokuwa mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha Ufaransa."

Alipoulizwa kuhusiana na mawazo ya Makelele, Kante alisema: "Nafikiri ni vizuri kusikiliza ushauri unaotolewa na aina ya mchezaji kama Makelele, natakiwa kusikiliza na kuufanyia kazi ipasavyo.

"Siwezi kuahidi kuwa nitaweza kufanya kile ambacho kila mtu atanitaka nifanye, lakini ni vema kusikiliza ushauri kutoka kwa mchezaji wa aina yake na kutoka kwa uongozi pamoja na meneja kwa ujumla.

"Nataka kuboresha kiwango changuna niko nafanya kila liwezekanalo ili kuimarika hivyo nasikiliza ushauri na kujaribu kuufanyia kazi. Kama nikifanya, ni sawa tu, lakini najaribu kutoitumia nguvu kubwa sana kwa hilo pekee."
N'golo Kante amjibu Claude Makelele N'golo Kante amjibu Claude Makelele Reviewed by Zero Degree on 8/26/2017 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.