Loading...

Multichoice Tanzania yashusha bei ya vifurushi vyake vyote

Balozi maalum wa DStv, Nancy Sumari akitoa zawadi ya DStv kwa waliojitokeza wakati wa tukio hilo la kutangazwa kwa punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017
Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hususan vile vya bei ya chini.

Habari hiyo njema imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.

“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage.

Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema kumekuwa na punguzo la hadi asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv.

Amezitaja bei mpya za vifurushi vya DStv kuwa ni; Bei ya sasa kifurushi cha Premium TZS 184 000.00 huku bei ya punguzo ni TZS 169 000.00 asawa na asilimia 8.15%. Kwa kifurushi cha Compact Plus ambacho kilikuwa kinauzwa TZS 122 500.00, kwa sasa ni bei ya punguzo ni TZS 109 000.00, Kifurushi kingine cha Compact TZS 82 250.00 na kwa bei ya punguzo ni TZS 69 000.00.

Vifurushi vingine ni pamoja na Family TZS 42 900.00 na bei ta sasa ni TZS 39 000.00, Kifurushi cha Access (Bomba) TZS 19.975.00 huku bei ya sasa ikiwa ni TZS 19 000.00.

Maharage amebainisha kuwa, huko mtaani ‘vyuma vimekaza’, kwani hali ya kifedha imebana zaidi hivyo Multichoice imelisikia hilo na kuamua kuwapa wateja wote wa DStv ahueni kubwa, hivyo kwa hali hiyo sasa kwa wateja wa DStv, ‘Vyuma vimeachia’. alieleza Maharage.

Maharage amesisitiza kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza wateja wake na kuhakikisha kuwa inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale inapowezekana.

“Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”.

“Kipekee kabisa Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze nguvu kwenye kuinua vipaji vya vijana wetu wa kitanzania, tukasikia, tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo tumemdhamini mwanariadha wetu Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania inahofiwa kwenye ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu tunawasikiliza wateja wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza Watanzania” alisema Maharage.

Wakati habari hii ikiwa ni njema kwa watanzania wote, washabiki na wanazi wa kandanda wameonekana kufurahia Zaidi kwani kwa punguzo hilo kuwa wataweza kushuhudia ligi kuu ya uingereza PL pamaja na ligi nyingine kubwa ulimwenguni na makombe maarufu kama UEFA kwa bei nafuu zaidi.
Multichoice Tanzania yashusha bei ya vifurushi vyake vyote Multichoice Tanzania yashusha bei ya vifurushi vyake vyote Reviewed by Zero Degree on 8/29/2017 08:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.