Loading...

Kampuni ya GF Trucks yaimwagia Mbao FC mamilioni


Klabu ya Mbao FC imesaini mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na Kampuni ya GF Trucks and Equipment Limited wenye thamani ya Sh 140 milioni.


Kampuni ya GF Trucks inajihusisha na uuzaji wa vipuri vya magari, katika mkataba wake itawapatia Mbao basi lenye thamani ya Sh 70milioni pamoja na kutoa Sh 70 milioni nyingine kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa klabu hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kutia saini Ofisa Masoko wa GF Trucks and Equipment Ltd, Kulwa Bundala alisema kampuni hiyo imevutiwa mwenendo wa Mbao na kuamua kuidhamini.

"Tulikuwa tukiwafuatilia bila wao kujua, tunathamini mpira na ndio maana tumeona tuungane nao, tutawapatia basi lenye thamani ya Sh 70Milioni," alisema Bundala. 

Basi hilo wanategemea kulikabidhi baada ya mwezi mmoja.

Mwenyekiti wa Mbao Zefania Mjashi alisema si jambo dogo.

"Suala la usafiri ilikuwa changamoto, tunashukuru kwa udhamini huu ambao utatusaidia kuijenga Mbao ili itoe ushindani," alisema Mjashi. 

Mbao ilianza Ligi Kuu kwa kuichapa Kagera Sugar kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Kampuni ya GF Trucks yaimwagia Mbao FC mamilioni Kampuni ya GF Trucks yaimwagia Mbao FC mamilioni Reviewed by Zero Degree on 8/30/2017 12:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.