Loading...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine leo Ijumaa Tar 18, Agosti 2017


Rais John Magufuli leo Ijumaa amefanya uteuzi wa viongozi watatu katika nafasi mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Profesa Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (Tiper).

Profesa Mruma pia ni mtendaji mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania.

Pia, Rais Magufuli amemteua Profesa Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania.

Profesa Buchweshaija ni naibu mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Vilevile Rais Magufuli amemteua Profesa Evaristo Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).

Profesa Liwa amechukua nafasi ya Profesa Idrissa Mshoro ambaye amestaafu. Uteuzi wa viongozi hao umeanza Agosti 17, 2017
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine leo Ijumaa Tar 18, Agosti 2017 Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine leo Ijumaa Tar 18, Agosti 2017 Reviewed by Zero Degree on 8/18/2017 02:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.