Loading...

Ridhiwani amkumbuka Philemon Ndesamburo


Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amekutana na familia ya marehemu Philemon Ndesamburo na kuelezea namna mzee huyo alivyokuwa karibu naye.

Gazeti la Mwananchi linadai Ridhiwani amesema kuwa aliwahi kuambiwa na mzee huyo kuwa anatamani kumuona anakua kijana mwenye mapenzi kwa vijana wenzake.

Ndesamburo aliwahi kuwa mbunge wa Moshi mjini kwa tiketi ya Chadema na pia mwenyekiti wa chama hicho hadi alipofariki dunia miezi michache iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gazeti la Mwananchi, Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo baada ya kwenda kuhani msiba nyumbani kwa marehemu mjini Moshi.

Akizungunza na baadhi ya ndugu na jamaa marehemu Ndesamburo, Ridhiwani amesema alikutana mara ya kwanza ana kwa ana na kuzungumza na mzee huyo miaka kadhaa iliyopita alipokwenda Moshi kumuona babu yake aitwaye Mzee Semindu na pia alikutana naye tena kipindi cha Bunge la Katiba. "Namkumbuka sana, aliwapenda sana wabunge vijana na hata akiwaona wamekuwa kimya sana aliwauliza kuwa vipi mbona uko mpole leo?” amesema
Ridhiwani amkumbuka Philemon Ndesamburo Ridhiwani amkumbuka Philemon Ndesamburo Reviewed by Zero Degree on 8/16/2017 06:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.