Loading...

Sugu afunguka mazito


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema nchi inayumba kutokana na hofu inayojengeka miongoni mwa watu wanaoikosoa Serikali kukamatwa na vyombo vya dola jambo ambalo halina tija kwa mustakabali wa nchi inayopambanua kuwa na uchumi wa viwanda.

Mbali na hilo, Sugu alisema kitendo cha Rais John Magufuli kupiga marufuku vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kumekuwa na muingiliano wa shughuli za kisiasa na za kiserikali kwa madai kwamba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamekuwa wakivizia shughuli zinazofanywa na viongozi wa kiserikali.

Sugu amesema hayo juzi jioni kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Kata ya Iyela uliofanyikia Mtaa Maendeleo jijini hapa.


“Hivi sasa inchi inayumba ndugu zanguni, wenzetu CCM hawana sehemu ya kuzungumzia wamebakia kuvuruga shughuli za kiserikali kwa kuchomekea mambo yao, lakini kama hiyo haitoshi hofu imetanda kwa kila mmoja, kwa mfano jana (juzi) nimepigiwa simu nyingi sana toka viongozi wa usalama wa Serikali kuhusu mkutano wangu wa leo, sasa hawa watu wanaacha kufanya shughuli za kimaendelep wanabakia kutafuta nani anafanya nini au anataka kusema nini,” amesema Sugu. 

Amemuomba Rais Magufuli kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ili kuleta ustawi wa kidemokrasia vile vile kutoleta vitisho kwa wanaoikosoa Serikali.

Amesema: "Leo hii Jiji la Mbeya lipo chini ya Chadema, Meya na Mbunge ni Chadema tunatarajia kupata ukosoaji wa utendaji kazi wetu kutoka kwa CCM kupitia mikutano ya hadhara, lakini kwa vile ‘Bosi’ wao kawabania wanakosa mahala pa kutokosoa na hili ndugu zangu niwaambie inaendelea kuwadidimiza." 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda (Chadema) amesema pamoja na upinzani hususani Chadema kubana kila kona lakini aliwataka wananchi kutoyumbishwa wala kurudi nyuma kwani kila kitu kina mwisho.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi alisema Serikali imechukua vyanzo vyote vya mapato kutoka halmashauri na kuzifanya zishindwe kujiendesha, lakini akawataka wananchi kutovunjika moyo bali waendelee kuchapa kazi.

"Wameona hawana sehemu ya kutukamatia leo hii wamekimbilia kwenye vyanzo vya mapato kutoka kwenye halmashauri zetu wamechukua, lakini niseme tu pamoja na kutung’anya vyanzo vya mapato ya ndani sisi Chadema ndani ya miaka miwili hii tumefanikiwa kujenga madaraja 10 yanayounganisha jijini na maeneo pembezoni."

Source: Mwananchi
Sugu afunguka mazito Sugu afunguka mazito Reviewed by Zero Degree on 8/26/2017 05:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.