Tanzania ndio nchi pekee Afrika Mashariki na kati yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya kilimo
Hali hiyo imeelezwa kwenye mkutano uliowakutanisha wakurugenzi wa halmashari za wilaya, maafisa kilimo, wakulima, wasindikaji wa mazao ya kilimo pamoja na sekta binafsi, mkutano ulioandaliwa na baraza la kilimo na mifugo Tanzania (ACT) kwa lengo la kujadili hatima ya wakulima wadogo waweze kunufaika na kilimo.
Kufuatia mkutano huo mitazamo tofauti kutoka kwa wadau hao imejitokeza kuona hali ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo huku wengine wakitoa ushauri kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera za kilimo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa baraza la kilimo na mifugo Tanzania (ACT)Bi,Janet Bitegeko ameeleza mikakati ya baraza hilo juu ya uboreshaji wa sekta ya kilimo na mifugo nchini.
Source: ITV
Tanzania ndio nchi pekee Afrika Mashariki na kati yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya kilimo
Reviewed by Zero Degree
on
8/19/2017 10:10:00 AM
Rating: