Loading...

Video: Aubameyang ataja klabu anayotaka kujiunga nayo katika majira haya ya joto


Pierre-Emerick Aubameyang amethibitisha rasmi klabu ambayo angependa kujiunga nayo katika majira haya ya joto.

Aubameyang amekuwa akihusishwa na kujiunga na vilabu kama Arsenal, Chelsea na Liverpool ambavyo vinashiriki Ligi Kuu ya Uingereza.

Pia alipata ofa kubwa kutoka klabu ya Tianjin Quanjin.

Lakini inakuwa tofauti na matarajio ya wengi kwani yeye hataki kujiunga na klabu yoyote kati ya hizo, badala yake ameweka wazi kupitia Instagram klabu anayotaka kuichezea kama ataondoka Dortimund.

Aubameyang alirusha kipande kifupi cha video akiambiwa na shabiki wa kituo cha 'Rossoneri': “Njoo AC Milan”.

Aubameyang akajibu hivi, kama ambavyo ilionekana kwenye video hiyo: “Hata mimi ninataka, lakini wao wamelala sasa nitafanya nini?”


Dortmund wamekuwa na furaha kusikia ofa mbali mbali zikitolewa kwa ajili ya Pierre-Emerick Aubameyang lakini bado haijajitokeza klabu yoyote kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya kumsajili nyota huyo.
Video: Aubameyang ataja klabu anayotaka kujiunga nayo katika majira haya ya joto Video: Aubameyang ataja klabu anayotaka kujiunga nayo katika majira haya ya joto Reviewed by Zero Degree on 8/14/2017 03:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.