Loading...

Video: Liverpool yafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA] kwa kuichapa Hoffenheim goli 4-2


Liverpool walionyesha mchezo mkali wa kushambulia na kuwazidi nguvu wapinzani wao katika michuano ya muondoano ya kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano na kuondoka na ushindi wa 4-2, na jumla ya 6-3.

Ushindi wao dhidi ya Hoffenheim umehakikisha kwamba kwamba mara ya kwanza England itawakilishwa na klabu tano katika hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Liverpool walikuwa wakiongoza 2-1 kutoka kwa mechi ya kwanza na walihakikisha mambo hayawezi kuwageuka kwa kufunga mabao matatu dakika 20 za kwanza za mechi.

Emre Can aliwafungia la kwanza kabla ya Mohamed Salah kuongeza la pili.

Can alifunga la pili kutoka kwa krosi ya Roberto Firmino sekunde 143 baadaye kabla ya nguvu mpya wa Hoffenheim Mark Uth, aliyeingizwa dakika ya 24 kuokoa jahazi la klabu hiyo ya Ujerumani kukomboa bao moja.

Mshambuliaji wa zamani wa Hoffenheim, Firmino, hata hivyo alihakikisha Liverpool wanaibuka wababe kwa kufunga baada ya mapumziko Jordan Henderson alipompokonya mpira nahodha wa wapinzani wao Kevin Vogt.

Wajerumani hao, ambao walimaliza wa nne katika Bundesliga msimu uliopita, hawakufa moyo na waliokomboa bao jingine Sandro Wagner alipofunga kwa kichwa kutoka kwa krosi ya Andrej Kramaric.

Liverpool pamoja na Chelsea, Tottenham, Manchester City na Manchester United watawafahamu wapinzani wao hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya droo itakapofanywa baadaye leo Alhamisi saa moja jioni saa za Afrika Mashariki.

Baada ya kwenda mechi mbili za kwanza bila kushindwa, kwa kutoka sare na Watford na kuilaza Crystal Palace, Liverpool watakuwa wenyeji wa Arsenal uwanjani Anfield siku ya Jumapili jioni.


Video: Liverpool yafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA] kwa kuichapa Hoffenheim goli 4-2 Video: Liverpool yafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA] kwa kuichapa Hoffenheim goli 4-2 Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 10:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.