Loading...

Bavicha wapingana na Jeshi la Polisi


BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limesema kuwa wataendelea na mpango wao wa kumuombea dua Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu kesho Jumapili, Septemba 17.

Bavicha wamedai leo kwamba, zuio la Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alilolitoa jana Ijumaa kuwataka wasifanye mikusanyiko isiyo halali, haliwahusu kwa sababu wao hawafanyi maandamano kama alivyoeleza yeye.

Mapema jana, Jeshi hilo lilipiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanywa na BAVICHA ili kumuombea Tundu Lissu ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi, Kenya baada kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa vibaya ma watu wasiojulikana nyumbani kwake Aread D, Dodoma wiki iliyopita.
Bavicha wapingana na Jeshi la Polisi Bavicha wapingana na Jeshi la Polisi Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 01:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.