Loading...

Bilioni 86 zatengwa kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini


Naibu waziri ofisi ya rais tamisemi mhe selemani jafo amesema serikali imetenga shilingi bilioni 86 kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini huku maeneo ya kipaumbele yakiwa ni jengo la upasuaji wodi za kinamama na watoto maabara na nyumba za watumishi ili kuboresha utoaji huduma na kupunguza vifo vya kinamama na watoto.

Ukarabati huo utaanza mapema iwezekanavyo na hadi kufikia december 30 mwaka huu utakamilika huku wakuu wa mikoa na wilaya wakitakiwa kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi, kusimamia fedha hizo na makatibu tawala wakitakiwa kuwasilisha taarifa za kila mwezi kuhusu maendeleo ya ukarabati huo.

Fedha hizo zimetolewa na benki ya dunia kwenda wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dola milioni 66 balozi wa canada kwenda tamisemi dola milioni 22 na fedha za ndani zilizovuka mwaka wa fedha 2016/2017 bilioni 12.5 ambapo kila kituo kitapata shilingi milioni 500.

Kwa upande wao wakazi wa mji wa dodoma wamepongeza hatua hiyo ya serikali kwani itaboresha huduma za afya hasa maeneo ya vijijini ambayo yana uhitaji mkubwa.

Source: ITV
Bilioni 86 zatengwa kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini Bilioni 86 zatengwa kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini Reviewed by Zero Degree on 9/15/2017 12:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.