Loading...

Chelsea yaingia matatani kwa kukiuka taratibu za usajili


Chelsea wanafanyiwa uchunguzi na Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) kwa kukiuka taratibu za usajili wa wachezaji wenye umri mdogo.

FIFA wamethibitisha kwamba wameanza kuifanyia uchunguzi klabu ya Chelsea juu ya suala la kusajili wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 kutoka nje.

Shirikisho hilo sasa liko linafanya uchunguzi juu ya suala hilo. Ikumbukwe pia Atletico Madrid wako kifungoni kufuatia kufungiwa na shirikisho hilo kwa kukiuka utaratibu. Walijaribu kukata rufaa lakini haikusaidia.

Real Madrid pia waliadhibiwa mwaka uliopita, lakini adhabu yao ilipunguzwa kutoka kufungiwa kusajili kwa misimu miwili hadi mmoja.

Ingawa suala la Chelsea linaaminika kuwa dogo ukilinganisha na hayo ya klabu hizo mbili za Spain, itategemea na adhabu itakayotolewa na FIFA katika uamuzi wao wa mwisho baada ya upelelezi kukamilika.
Chelsea yaingia matatani kwa kukiuka taratibu za usajili Chelsea yaingia matatani kwa kukiuka taratibu za usajili Reviewed by Zero Degree on 9/20/2017 09:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.