Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar kuwania tuzo ya mchezaji bora
Ronaldo aliisaidia Real Madrid kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufanikiwa kufunga magoli 12.
Messi na Neymar walifanikiwa kulibakisha taji la Copa del Rey Barcelona wakati huo huo Messi aliibuka mfungaji bora wa La Liga kwa kufunga magoli 37 msimu uliopita.
Nahodha wa Juventus, Gianluigi Buffon ameorodheshwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya Golikipa bora baada ya kuiongoza Juventus kubeba taji la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa mara ya sita mfululizo na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Buffon alijumuishwa na Keylor Navas wa Real Madrid pamoja na goli kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer.

Zinedine Zidane (Real Madrid), Antonio Conte (Chelsea) na Massimiliano Allegri (Juventus) walikuwa kwenye orodha ya mwisho ya wanaowania tuzo wa Kocha bora kwa wanaume.
Kwa upande mwingine, Mshambuliaji wa Venezuela, Deyna Castellanos, Carli Lloyd (America), na Lieke Martens, iliyeisaidia Uholanzi kwenye michuano ya kombe la Euro mwaka 2017 ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kike.
Tuzo hizo zitatolewa London nchini Uingereza mnamo tarehe 23, Octoba 2017.
Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar kuwania tuzo ya mchezaji bora
Reviewed by Zero Degree
on
9/23/2017 12:10:00 AM
Rating: