Loading...

Dele Alli afungiwa mechi moja ya kimataifa


Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amepigwa marufuku kutoshiriki mechi moja ya kimataifa kufuatia hatua yake ya kuinua kidole cha kati wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atashiriki mechi dhidi ya Lithuania siku ya Jumapili.


Alli alisema kuwa ishara hiyo ilimlenga aliyekuwa mchezaji mwenza wa Spurs Kyle Walker wakati wa dakika ya 77 ya ushindi wa 2-1 katika kundi F.

Kisa hicho kilitokea baada ya Alli kupigwa kumbo na beki wa Slovakia Martin Skrtel huku refa Clement Turpin akionyesha ishara ya mchezo uendelee.

Ilionekana kana kwamba Alli alimuonyesha ishara hiyo ya kidole cha kati afisa huyo ambaye pia walirushiana maneno alipotolewa nje dakika ya 93.
Dele Alli afungiwa mechi moja ya kimataifa Dele Alli afungiwa mechi moja ya kimataifa Reviewed by Zero Degree on 9/30/2017 07:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.