Habari muhimu kwa wateja wa Airtel
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, imetangaza neema kwa wateja wake ambapo bidhaa mbalimbali zinazopatikana kwenye maduka yao, zimeshuka bei kwa kiwango kikubwa, jambo litakalomnufaisha mteja hasa katika kipindi hiki kigumu cha kiuchumi.
Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Celina Njuju, amesema bidhaa zilizopunguzwa bei ni pamoja na modem za kisasa na simu, ambapo mteja atakayehitaji kunufaika na ofa hizo, anatakiwa kutembelea maduka ya Airtel yaliyopo kila kona nchini.
Aliongeza kuwa Wingle USB Modem kwa ajili ya intaneti, ambayo awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 60,000, sasa itakuwa ikipatikana kwa shilingi 45,000 pamoja na kifurushi cha intaneti cha bure cha 5GB. Modem hii inaweza kutumiwa na watu mpaka kumi kwa wakati mmoja na inawafaa zaidi wafanyakazi wa maofisini, wafanyabiashara na wanafunzi.

“Tunataka wateja wafaidi thamani ya fedha zao, siku zimepita ambapo Watanzania walikuwa wanaenda madukani na kununua bidhaa feki kwani kwa sasa tunazo bidhaa halisi kabisa ambazo zinapatikana kwa bei nafuu,” alisema Njuju.
Aliongeza kuwa Wingle USB Modem kwa ajili ya intaneti, ambayo awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 60,000, sasa itakuwa ikipatikana kwa shilingi 45,000 pamoja na kifurushi cha intaneti cha bure cha 5GB. Modem hii inaweza kutumiwa na watu mpaka kumi kwa wakati mmoja na inawafaa zaidi wafanyakazi wa maofisini, wafanyabiashara na wanafunzi.
“Pia imetoa punguzo la bei kwa simu ya Magnus Bravo Z11 ambapo hapo awali ilikuwa inauzwa shilingi 79,000 lakini kwa sasa inapatikana kwa shilingi shilingi 69,000 ikiwa na kifurushi cha bure cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na SMS 300 kwa muda wa miezi sita. Pia kuna punguzo kwenye simu ya Huawei Y3C ambapo hapo awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 140,000 lakini sasa itakuwa ikipatikana kwa shilingi 100,000, ikiwa na kifurushi cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na SMS 300 kwa muda wa miezi sita,” alisema Njuju na kuongeza:
“Wateja pia watajipatia simu aina ya FERO 280 kwa shilingi 30,000 kutoka bei ya awali ya shilingi 38,000 ambapo itakuja na 150MB, dakika 150 kupiga Airtel kwenda Airtel na SMS 150 kwa muda wa miezi mitatu. Natoa wito kwa wateja wa Airtel kujitokeza na kufaidika na punguzo la bei ya bidhaa hizi kwenye maduka yote ya Airtel nchi nzima kwani muda wa punguzo ni mdogo.”
Habari muhimu kwa wateja wa Airtel
Reviewed by Zero Degree
on
9/25/2017 11:17:00 PM
Rating: