Loading...

Wachezaji wengine wawili wanaotegemewa kuondoka Chelsea mwezi Januari


Kulingana na ripoti mbali mbali zinazoendelea kutolewa mitandaoni, wachezaji wengine wawili wa Chelsea wanategemewa kuondoka Stamford Bridge mwezi Januari.

Mmoja kati ya wawili hao ni Willian. Ripoti zinadai Mbrazili huyo amekuwa na wakati mgumu kutetea nafasi yake ndani ya kikosi cha kwanza cha Antonio Conte na anaweza kupewa nafasi ya kuondoka kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ameonekana akiitumikia vyema klabu yake kwa takribani michezo 34 msimu uliopita na michezo 15 tu kati ya hiyo ndiyo aliyofanikiwa kuanza na kikosi cha kwanza, hiyo ikiwa na maana kwamba, endapo kila mchezaji atakuwa na afya ya kucheza ni vigumu kwake yeye kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kujituma kwake kwenye Ligi ya Mabingwa inaweza kuwa fursa nzuri kwake kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Antonio Conte, lakini endapo ataendelea kukaa benchi kwa kipindi hiki hadi kufika January basi taarifa za uvumi wa yeye kuondoka Chelsea zitaendelea kugonga vichwa vya habari.

Mchezaji mwingine anayetajwa ni Micy Batshuayi, ambaye pamoja na kuondoka kwa Diego Costa Chelsea, bado anajikuta kwenye wakati mgumu kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza, uwezekano wa kuchaguliwa na Conte katika kila mechi ni mdogo baada ya kuwasili kwa Alvaro Morato, ambaye anaonekana kuwa na nafasi kubwa kwenye mipango ya muitaliano huyo hivyo kumfanya atafute sehemu nyingine anakoweza kupata nafasi ya kutosha ndani ya kikosi cha kwanza.
Wachezaji wengine wawili wanaotegemewa kuondoka Chelsea mwezi Januari Wachezaji wengine wawili wanaotegemewa kuondoka Chelsea mwezi Januari Reviewed by Zero Degree on 9/25/2017 02:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.