Marekani: Kisa wimbo wa taifa, Rais Donald Trump atofautiana na wanamichezo
Baltimore Ravens |
Kupitia mtandao wa kijamii siku ya Ijumaa, Rais wa Marekani, Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kulaani walichokifanya wachezaji kukaidi kuheshimu wimbo wa taifa. |
Wachezaji wa timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars za marekani nimiongoni mwa wanamichezo ambao wameonyesha kutofurahia na sera za Trump baada ya kushindwa kuheshimu wimbo wa taifa wa marekani ulipokuwa ukipigwa katika uwanja wa Wimbley ikiwa ni inshara ya kuonyesha umoja wa kumpinga Rais huyo.
Mmmiliki wa timu ya Jaguars, Shahid Khan ambaye alitoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 740,000 katika kumuunga mkono Trump wakati wa kampeni aliungana na wachezaji wake katika kupinga yanayo fanywa na Rais huyo.

Mfalme wa mchezo wa basketbaal, Steph Curry yeye alianika hisia zake wazi kwakusema kuwa kamwe hatokanyaga Ikulu ya Marekani, White House ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hisia zake za kupinga sera hizo huku akiamini kuwa kwa kufanya kitendo hicho kitakuwa mbolea ambayo italeta mafanikio kwa wengine kufuata nyayo zake kwakuwa anataka kuionyesha dunia hisia zake juu ya utendaji kazi wa raisi huyo.
Marekani: Kisa wimbo wa taifa, Rais Donald Trump atofautiana na wanamichezo
Reviewed by Zero Degree
on
9/25/2017 01:23:00 PM
Rating: