Loading...

Hassan Banyai aachia ngazi Njombe Mji


Kocha wa Njombe Mji, Hassan Banyai amejiuzulu nafasi yake kwa sababu aambazo hakutaka kuziweka wazi.

Gazeti la Mwananchi linadai kwamba, Uamuzi wa Banyai umekuja saa chache baada ya kuachwa kwenye msafara wa timu hiyo kutokea Mbeya kwenda Njombe kutokana na kufungwa na Mbeya City 1-0.

"Nimeamua kuachia ngazi na sababu za kufanya hivyo nitaziweka hadharani kwenye mkutano wangu na waandishi wa habari," alisema Banyai. 

Kujiuzulu kwa Banyai kumethibitishwa na klabu hiyo kupitia taarifa yake kwa wanahabari. 

" Uongozi wa Njombe Mji unapenda kuwataarifu wanafamilia wa soka kuwa kocha mkuu ndugu Hassan Banyai ameamua kuachia ngazi kwa hiari yake muda mfupi uliopita," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Hassan Banyai aachia ngazi Njombe Mji Hassan Banyai aachia ngazi Njombe Mji Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 06:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.