Loading...

Haya ndio Mataifa 8 yaliyofuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2018


MICHUANO ya Kombe la Dunia itafanyika mwakani nchini Urusi na tayari mambo yameanza kuwa mazuri kwa baadhi ya nchi, lakini zingine mambo yao siyo sawa. Hii ndiyo michuano mikubwa zaidi duniani na yenye rekodi kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka.

Tayari kwenye fainali za mwakani, mataifa nane yameshakata tiketi ya kwenda Urusi na yameshaanza kufikiri kuwa yatapangwa na nani kwenye hatua ya makundi ya fainali hizo lakini kati ya yote hakuna hata moja kutoka Afrika. Mbali na mataifa hayo, kuna timu ya Urusi ambayo imepewa tiketi ya moja kwa moja kushiriki kwa kuwa ndiyo waandaaji wa fainali hizo, hivyo kufanya mpaka sasa kuna timu nane, lakini saba ndizo zilizofuzu kwa, Urusi kutoa jasho mpaka sasa.

Wanaume hao saba ni mabingwa wa kihistoria Brazil na Ubelgiji, na engine ni Iran, Mexico, Japan, Saudi Arabia na Korea Kusini ambao wanafuzu fainali zao za tisa mfululizo. Swali la kujiuliza ni kwamba wanawezaje kufuzu kwa fainali hizi mapema namna hii wakati inaamini- k a kuwa ni vigumu sana k u p a t a nafasi hiyo adimu? Na je, mastaa wao ni kina nani? Fuatilia hapa.



URUSI: Hawa wamepewa nafasi ya moja kwa moja lakini hawana kiwango cha kutisha na hata kwenye michua- no ya Kombe la Mabara hawakuonyesha kiwango chochote cha maana wakiondolewa kwenye hatua ya kwanza. Walipoteza michezo yote dhidi ya Mexico na Ureno baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya vibonde New Zealand.

Hii inaonyesha kuwa wanatakiwa kufanya kazi kubwa ili angalau kufuzu kwa hatua ya makundi. Mchezaji wao watakayemtegemea ni kipa Igor Akinfeev, ambaye atakuwa nahodha wa timu hiyo.


UBELGIJI: Ubelgiji imekuwa timu ya kwanza kutoka Bara la Ulaya kufuzu kwa michuano hii mikubwa duniani wakiwa bado wana michezo miwili mkononi.

Inatajwa kama timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kufika robo fainali mwakani wakiwa hawakufuzu kwa fainali mbili zilizopita. Ukiacha England kama itafuzu, hii ndiyo nchi ambayo itakwenda kwenye fainali hizi ikiwa na wachezaji 

Hawa wamefuzu kutokana na kuwa na mastaa kibao wakiwemo Moussa Dembele, Marouane Fellaini, Christian Benteke, Romelu Lukaku, Kevin De Bruyne na Eden Hazard. Inatajwa kama timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kufi ka robo fainali mwakani wakiwa hawakufuzu kwa fainali mbili zilizopita.

Ukiacha England kama itafuzu, hii ndiyo nchi ambayo itakwenda kwenye fainali hizi ikiwa na wachezaji wengi kutoka Ligi Kuu England.

BRAZIL: Brazil ilikuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali hizo, walifanya hivyo Machi, mwaka huu na siku zote wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa na sasa bado wana nafasi hiyo.

Wakiwa na wachezaji wengi mahiri na vijana, Brazil ambao wametwaa ubingwa huo mara tano wanapewa tena nafasi ya kufanya mambo makubwa mwakani.

Walifanikiwa kutwaa ubingwa huo mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002, lakini wanakumbuka kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani kwenye fainali zilizopita ambazo zilifanyika nchini kwao. Staa wanayemtegemea ni Neymar ambaye kwa sasa anaichezea PSG akiwa mchezaji ghali zaidi duniani.

MEXICO: Hii ni timu ambayo ina kasi ya hali ya juu sana ikiwa uwanjani, wenyewe hadi sasa hawajafungwa mchezo hata mmoja kwenye michezo yao ya kufuzu. Ni timu inayoheshimika kwa kuwa imefanikiwa kufi ka kwenye hatua ya mtoano kwenye fainali sita za Kombe la Dunia zilizopita. Staa wao atakuwa Hirving Lozano, mshambuliaji ambaye ameonyesha kasi nzuri ya kupachika mabao.

IRAN: Huwezi kuzipa nafasi kubwa sana timu kama Iran kuweza kufanya vizuri kwenye fainali hizo, lakini elewa kwamba nao wameshafuzu wakiwa wanafundishwa na kocha Carlos Queiroz ambaye amewahi kuwa msaidizi wa Alex Ferguson. Wamefuzu wakiwa wamecheza michezo 12 bila kuruhusu bao kuonyesha kuwa ni timu yenye safu imara sana ya ulinzi. Hii ni mara yao ya tano kwenye historia wanafuzu lakini mara zote wamewahi kushinda mchezo mmoja tu dhidi ya Marekani kwa mabao 2-1, mingine yote walifungwa na kuondolewa mapema. 

Ramin Rezaeian, ndiye staa wao wanayemtegemea kuwa atawabeba.

KOREA KUSINI: Korea Kusini wamefuzu wakiwa na kumbukumbu kubwa zaidi ya kufi ka hatua ya nusu fainali mwaka 2002, walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo. Mwaka huu wamekata tiketi wakiwa wameshinda michezo minne tu wakisubiri kuona kama wanaweza kufanya maajabu tena. Staa wao ni Son Heung-min, ambaye amekuwa kwenye kikosi cha Tottenham lakini akiwa anatajwa kuwa staa sana kwenye timu hiyo kwa miaka ya hivi karibuni.

JAPAN: Hawa wamefuzu kwa kila fainali kuanzia mwaka 1998, lakini wamekuwa hawaonyeshi kiwango cha juu uwanjani, labda wanaweza kuwika mwakani. Wanawategemea mastaa wao kama Keisuke Honda pamoja na staa wa Borussia Dortmund, Shinji Kagawa.

SAUDI ARABIA: Majabu ni kwamba hizi zitakuwa fainali zao za kwanza kabisa tangu mwaka 2006 walipofuzu na kuchapwa mabao 8-0 na Ujerumani ambapo ni kipigo kikubwa kwao kwenye Kombe la Dunia. Wamekuwa wakitajwa kuwa wana ligi imara sana barani Asia, lakini siyo timu ambayo inaweza kuleta ushindani mkubwa. Heshima yao inaonyesha kuwa wamewahi kushinda michezo miwili tu ya Kombe la Dunia, tangu wameanza kushiriki na mmoja ni ule dhidi ya Ubelgiji waliposhinda 2-1. Staa wao ambaye atawabeba ni Nasser Al Shamrani, huyu alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Bara la Asia mwaka 2014.
Haya ndio Mataifa 8 yaliyofuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2018 Haya ndio Mataifa 8 yaliyofuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2018 Reviewed by Zero Degree on 9/13/2017 07:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.