Kisa kufuta matokeo ya Urais, Mbunge aomba jaji mkuu afukuzwe kazi Kenya
Mbunge wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu |
Jaji mkuu, David Maraga |
Mbunge huyo wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu amewasilisha ombi lake mbele ya tume ya huduma za majaji akidai kwamba jaji Maraga alihusika katika kufanya makosa.
Akihutubia vyombo vya habari, mbunge huyo anadai kwamba Jaji huyo ''aliwashinikiza'' wenzake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais Uhuu Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria mnamo tarehe 1 Septemba.
Wambugu amefananisha ubatilishwaji wa matokeo hayo ya urais na mapinduzi ya majaji na sasa anataka nia ya jaji Maraga kuchunguzwa.
Wabunge wa chama cha Jubilee na rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiukosoa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo na wameendelea na kuwataja majaji hao kuwa ''wakora''.
Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa urais wa Oktoba 17, uamuzi huo wa majaji na sababu zao utaangaziwa upya.

Reviewed by Zero Degree
on
9/14/2017 08:41:00 PM
Rating: