Loading...

Majambazi watano na mganga mmoja wa kienyeji wamekamatwa na Jeshi la Polisi Dar


Jeshi la polisi Kandamaalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi lililokuwa limepangwa kufanyika katika jengo la Mkuki Kamata ambapo majambazi watano na mganga mmoja wa kienyeji wanashikiliwa na jeshi hilo.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema tukio hilo lilitokea septemba 3 mwaka huu watuhumiwa wakiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu ikiwemo mitungi midogo ya gesi ya kufungualia mageti na wote wamekiri kudhamiria kufanya tukio hilo.

Aidha jeshi hilo limetoa ufafanuzi taarifa za kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama cha CHAUMA Hashimu Rungwe toka agosti 28 mwaka huu ambae pia ni wakili kwa tuhuma za utapeli hata hivyo amepatiwa dhamana agosti 5 mwaka huu.

Kamishna Mambosasa ameendelea kutoa wito kwa madereva kutii sheria za barabarani na kubaini kwa kipindi cha siku saba wamekusanya zaidi ya milion mia nne kutokana na faini za makosa ya barabarani.
Majambazi watano na mganga mmoja wa kienyeji wamekamatwa na Jeshi la Polisi Dar Majambazi watano na mganga mmoja wa kienyeji wamekamatwa na Jeshi la Polisi Dar Reviewed by Zero Degree on 9/07/2017 11:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.