Loading...

Alvaro Morata aweka wazi kilichomfanya aondoke Real Madrid


Mchezaji mpya aliyesajiliwa na Chelsea, Alvaro Morata amesema alikuwa amechoka na kuwa mchezaji wa ziada katika benchi la Real Madrid.

Morata alikuwa mchezaji wa pili kwa kuwa na magoli mengi Real Madrid msimu uliopita akiwa nyuma ya Cristiano Ronaldo, hata hivyo, alijikuta akitumika kama mchezaji wa ziada kwenye safu ya ushambuliaji akiwa mbadala wa mshambuliaji Karim benzema ambaye alionekana kupewa nafasi kubwa katika safu hiyo.

Alifanikiwa kuanza katika michezo 19 tu kwenye michuano yote ambayo Madrid ilishiriki, hivyo kushawishika na ofa ya Chelsea ambapo ilihisi atapata nafasi ya kutosha uwanjani.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane alijaribu kumshawishi Morata abakie lakini ikashindikana.

Lakini matamanio ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kung'ara katika safu ya ushambuliaji kwenye timu yakeya taifa wakati wa kombe la dunia mwakani kulimfanya kwenda Chelsea ili kujiweka tayari kwa ajili ya mashindano hayo.



“Zidane alitaka mimi nibakie na nilikuwa na furaha pale Madrid,” Morata alisikika akiiambia Daily Mail. “Lakini nisingeweza kubakiwa na kuwa mchezaji wa akiba. 

“Inafikia hatua mtu unataka kucheza, kukua zaidi kisoka, na kuondokana na benchi.

“Ni kuhusu suala zima la kujisikia vizuri mahali ulipo. Sitaki kuwa mtu wa kutazama wenzangu huku nikiwa benchi. Nina malengo yangu pia nina njaa ya mafanikio.

“Kwa Spain, kadri nichezavyo, ndivyo navyopata nafasi ya kufunga magoli mengi zaidi, na hiyo ni fursa kubwa sana kwangu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye Kombe la Dunia mwakani.”

Morata amefanikiwa kuanza vizuri maisha mapya katika klabu ya Chelsea kwa kupachika mabao matatu ndani ya michezo mnne ya ligi kuu.
Alvaro Morata aweka wazi kilichomfanya aondoke Real Madrid Alvaro Morata aweka wazi kilichomfanya aondoke Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 01:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.