Loading...

Mwakyembe apiga marufuku Tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania

Dkt. Harrison Mwakyembe
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku uandaaji na uendeshwaji wa mashindano ya urembo (Miss Tanzania) na tuzo za muziki hapa nchini kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano hayo.

Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji wa hali ya juu ambapo kwenye utoaji wa tuzo kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu na mitafaruku.

Ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipelekwe ofisini kwa waziri huyo.

”Kwa sasa tutakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo, lakini tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha tu!”, alisema Mwakyembe.

Kwa mara ya mwisho mashindano ya za Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016 ambapo ilichukua takribani miezi 6 kwa Kamati ya shindano la Urembo la Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake.

Kwenye tuzo za muziki waziri Mwakyembe amesema tuzo hizo zinahitaji marekebisho kwani zilikuwa zikitegemea watu wachache kiasi kwamba wakinuna basi hakuna tuzo.
Mwakyembe apiga marufuku Tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania Mwakyembe apiga marufuku Tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania Reviewed by Zero Degree on 9/25/2017 11:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.