Loading...

Pogba hatarini kuikosa mechi ya Manchester United dhidi ya Everton wikendi ijayo


Pogba alijikuta akiisubiria Ligi ya Mabingwa kwa karibuni mwaka mmoja hivi tangu ajiunge na Manchester United, na hata hivyo, amefanikiwa kuichezea timu yake kwa takribani dakika 18 tu.



kiungo huyo wa Ufaransa alipata majeraha ya mguu mnamo dakika ya 15 katika mechi ya ufunguzi hatua ya makundi kati ya Manchester United dhidi ya FC Basel na kushindwa kuendelea kufuatia majeraha hayo.


Fellain ndiye aliyeingia uwanjani badala ya Pogba na kuifungia timu yake goli la kuongoza, lakini ikumbukwe pia, Pogba alikosa michezo kadhaa katika msimu uliopita kwa majeraha ya aina hiyo.

Mechi ijayo ya Manchester united itakuwa dhidi ya Everton, ambapo Wayne Rooney atakuwa anakutana na timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza kama mpinzani tangu kuondoka kwake, wakati huo huo Pogba akiwa hatarini kuikosa mechi ya hiyo itakayochezwa wikendi ijayo Old Traford.
Pogba hatarini kuikosa mechi ya Manchester United dhidi ya Everton wikendi ijayo Pogba hatarini kuikosa mechi ya Manchester United dhidi ya Everton wikendi ijayo Reviewed by Zero Degree on 9/13/2017 12:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.