Loading...

Rais Magufuli amjulia hali Meja Jenerali mstaafu aliyepigwa risasi


Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo,Jijini Dar es Salaam nakumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mritaba aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meja Jenerali Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mbali na kumjulia hali Meja Mritaba Rais Magufuli pia aliwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali hiyo.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wamagonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen.Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni natumboni.

Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe.RaisMagufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen.Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwaajili ya kupata matibabu.

Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya jeshi Lugalo kwa huduma zamatibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Rais Magufuli amjulia hali Meja Jenerali mstaafu aliyepigwa risasi Rais Magufuli amjulia hali Meja Jenerali mstaafu aliyepigwa risasi Reviewed by Zero Degree on 9/12/2017 05:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.