Loading...

Serikali kuajiri zaidi ya watumishi 11,000

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki amefunguka na kusema serikali inampango wa kuajiri zaidi ya watumishi elfu kumi na moja ambao watakwenda kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wenye vyeti feki.

Waziri Kairuki amesema hayo leo bungeni kufuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mh Ester N. Matiko kutaka kufahamu mpaka sasa serikali imeajiri jumla ya watumishi wangapi baada ya kuwatumbua watumishi wenye vyeti feki zaidi ya elfu tisa jambo ambalo limeleta athari kubwa kwenye sekta ya elimu na afya.

"Kwanza kabisa kama nilivyoeleza tumetoa vibali vya ajira zaidi ya elfu kumi na moja kwa upande wa ualimu tayari Wizara ya elimu imeanza zoezi la kutambua, wanatuma vyeti wale ambao walikuwa ni wahitimu na wanaostahili baada ya hapo watahakikiwa na kuweza kuingia katika ajira, ukiangalia katika walimu kwa ujumla wake katika ku replace watumishi ambao wameondoka ni zaidi ya walimu 3,012 wataajiri katika zoezi hilo lakini pia sekta ya afya tutaajiri zaidi ya watumishi 3152 hii ni katika kuziba pengo la walioghushi vyeti feki", alisema Kairuki.

Waziri Kairuki amesema kuwa idadi hii ya watumishi zaidi ya elfu sita ambao watapata ajira serikalini kuziba pengo la watumishi walioacha kazi kwa vyeti feki halihusiani na ajira zaidi ya elfu hamsini ambazo serikali ilitangaza kuzitoa.

"Baada ya hapo katika mwaka wa fedha 2017/2018 ajira bado zipo pale pale 52,436 kutokana na uwezo wetu wa kibajeti", alisisitiza Kairuki.
Serikali kuajiri zaidi ya watumishi 11,000 Serikali kuajiri zaidi ya watumishi 11,000 Reviewed by Zero Degree on 9/06/2017 12:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.