Serikali kuunda kikosi kazi kukabiliana na vitendo vya uharifu wa kutumia silaha
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi |
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi leo bungeni wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mkoani Twahir Mohamed (CUF) alipouliza ni kwa nini Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lisihusishwe katika kukomesha matumizi ya silaha na mauji ya raia wasiokuwa na hatia nchini huku akitolea mfano kwa tukio la shambulio la Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mirataba pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambao wote walishambuliwa na risasi katika siku tofauti ndani ya mwezi huu.
Amesema katika kufanikisha hilo wataunda kikosi kazi ambacho kitahusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama ambacho kitafanya kazi kwa kushirikiana ili kumaliza vitendo hivyo ambavyo kwa siku za karibuni vinaonekana kushamiri baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata kushambuliwa na watu wenye silaha hizo.
“Swala la kuimarisha usalama na amani ya nchi yetu ni la kila Mtanzania hata hivyo jeshi la nchi ndiyo lenye jukumu la kulinda mipaka ya kimaitafa na kuimarisha amani nchini na limekuwa likishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wadau kuhakikisha hakuna adui wa nje na ndani ambaye anahatarisha amani,
“Kazi ya jeshi ni ulinzi wa mipaka ila pale linapohitajika kusaidia mamlaka nyingine iwe ya kiraia au kiusalama linakuwa tayari kutoa msaada na kwahali ilivyosasa kutaundwa task force itakayojumuisha vyombo vyote vya usalama ili kuweza kulifanyia kazi tatizo hili la uvunjifu wa aamani na nataka niwahakikishie Watanzania jambo hili litafanywa vyema ili kuimarisha usalama wa nchi,” alisema Dkt. Mwinyi.
Serikali kuunda kikosi kazi kukabiliana na vitendo vya uharifu wa kutumia silaha
Reviewed by Zero Degree
on
9/14/2017 11:34:00 PM
Rating: