Loading...

Serikali yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra

Mamlaka zilikamata bahasha iliyokuwa na almasi ambayo hadi sasa haijaachiliwa
Shughuli zimeanza tena katika mgodi mkubwa zaidi wa madini ya almasi nchini Tanzania, licha ya mzozo na serikali ya Tanzania, ambayo ilikamata bahasha iliyokuwa na almasi kwenye uwanja wa ndege.

Shughuli katika mgodi wa Williamson zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa siku nne.

Wiki moja iliyopita hisa kwenye kampuni ya Uingereza ya Petra zilishuka kwa asilimia 7, baada ya almasi zake kuzuiwa kusafirishwa kutoka nchi Tanzania, ambapo pia wafanyakazi wake kadha walihojiwa na mamlaka za nchi hiyo.

Mamlaka zilikamata bahasha iliyokuwa na almasi ambayo hadi sasa haijaachiliwa.

Mazungumzo ya kampuni na serikali kuhusu suala hilo yanaendelea, kwa kujibu wa kampuni ya Petra.

Kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuchimba almasi nchi Tanzania inalaumiwa kwa kuzusha thamani ya almasi zake.

Serikali inasema kuwa Petra iliandika mzigo huo kuwa wa thamani ya dola milioni 14.6 wakati thahamia yake halisi ilikuwa dola milioni 29.5.

Petra ilikana madai hayo, ikisema kuwa serikali ndiyo inahusika kwa kuthibitisha thamani kama hiyo.

Mgodi wa Williamson ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania unamilikiwa na Petra kwa asilimia 25 huku serikali ya Tanzania ikimiliki asilimia 25.

Source: BBC Swahili
Serikali yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra Serikali yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 04:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.