Loading...

TANZIA: Golikipa aliyedaka kwenye mechi ya Simba Day afariki dunia


Golikipa wa Rayon Sports, Evariste Mutuyimana aliyedaka kwenye mechi dhidi ya Simba siku ya Simba Day jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa , amefariki dunia leo Jumanne kwenye Hospitali ya Kigali nchini Rwanda.

Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) limethibitisha kutokea kwa kifo cha mchezaji huyo, huku likitoa salamu za pole kwa klabu ya Rayon Sports.

Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo msimu wa mwaka 2016/17 akitokea Sofapaka FC ya Kenya.
TANZIA: Golikipa aliyedaka kwenye mechi ya Simba Day afariki dunia TANZIA: Golikipa aliyedaka kwenye mechi ya Simba Day afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 9/13/2017 12:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.