Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamis ya Tarehe 21 Septemba, 2017


Klabu za Chelsea na Everton zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa PSG, Edison Cavani. (Chanzo: Daily Mail)

Liverpool na Tottenham zaingia vitani kusaka saini ya kinda wa Werder Bremen David Philipp.

Manchester City wanaelekea kumaliza mazungumzo na Fernandinho kuhusu mkataba mpya, licha ya kwamba maelewano yanaonekana kuchukua muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa.

Arsenal wanafanya mpango wa kumsajili beki wa Marseille, Christopher Rocchia 
(Chanzo: The Sun)

Jose Mourinho anaumiza kichwa juu ya uwezekano wa kumbakisha Marouane Fellaini Manchester United ikiwa mbeligiji huyo bado hajasaini mkataba mpya hadi hivi sasa.

Kocha wa timu ya taifa ya Spain, Julen Lopetegui amemuambia Diego Costa kuchagua kumaliza sintofahamu iliyiyopo au kukosa kombe la dunia mwakani.

Arsenal wanaweza kumfuata upya Raheem Sterling mwezi Januari, wakimtumia Alexis Sanchez kama chambo.

Demarai Gray (Leicester City) amuonya Riyad Mahrez kwamba yuko tayari kuziba nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.

Fernando Llorente ameomba muda wa kutosha ili kutuliza akili pamoja kabla mashabiki wa Tottenham hawajaanza kumuandama. (Chanzo: Daily Mirror)

Chelsea, Manchester United hatarini kumkosa Leon Goretzka. Kiungo huyo wa Schalke anapendelea kujiunga na Barcelona. (Chanzo: Daily Star)

Akiwa anajiandaa kuivaa Rangers kwenye 'derby' yao ya kwanza msimu huu, meneja wa Celtic, Brendan Rodgers amefichua siri ya kwamba alijaribu kumsajili Graham Dorrans wa Swansea. (Chanzo: Daily Record)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamis ya Tarehe 21 Septemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamis ya Tarehe 21 Septemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 9/21/2017 10:21:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.