Loading...

Ufaransa kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024


Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imechagua mji mkuu wa ufaransa, Paris, kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024, na kuutunuku mji wa Los Angeles nchini Marekani kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2028.

Raisi wa kamati ya Olimpiki Thomas Bach (katikati) akitangaza wenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2024 na 2028 akiwa na meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo (kushoto) na meya wa mji wa Los Angeles Eric Garcetti (kulia)
Mwezi uliopita, kamati hiyo ilifanya maamuzi ya kuwa Olimpiki mbili za majira ya joto zitatolewa kwa wakati mmoja, baada ya miji kadhaa kuahirisha zabuni zao kutokana na wasiwasi wao kuhusu ukubwa, gharama, na utata wa kuandaa moja ya matukio makubwa kama hayo ya michezo duniani.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa uchaguzi wa mji wa Paris kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni ishara ya kutambuliwa kwa mji na nchi kitu ambacho kila Mfaransa anapaswa kusherehekea.
Ufaransa kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024 Ufaransa kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024 Reviewed by Zero Degree on 9/13/2017 11:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.