Loading...

Wabunge kutoa nusu ya posho yao ya siku moja kuchangia matibabu ya Tundu Lissu


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameridhia kutoa nusu ya posho yao ya siku moja kuchangia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia mmoja wa viongozi wa Chadema Mhe Tundu Lissu aliyepelekwa nchni Kenya kwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma.

Akizungumza katika kikao cha Bunge,Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai amesema tukio hilo ni aina yake haijawahi tokea mbunge kupigwa risasi wakati bunge likiwa linaendelea hivyo limewataadharisha wabunge wote ambapo ameomba wawe na subira ili vyombo vya dola viweze kulifanyia kazi.

Akielezea sababu za mheshimiwa Tundu Lissu kupelekwa nchni Kenya katika hospitali ya Agakhan kwa matibabu, Mhe Spika amesema ni chaguo la familia na si kwamba madaktari waliopo nchini hawana uwezo kutoa matibabu.

Aidha Mhe. Job ndugai amewata baadhi ya wabunge kuhacha kurusha maneno kwenye mitandao yanayotoa lawama katika taasisi mbalimbali ikiwemo Bunge na kuwataka kuhacha kuandika vitu vinavyoweza kuleta migongano katika jamii.

Source: ITV
Wabunge kutoa nusu ya posho yao ya siku moja kuchangia matibabu ya Tundu Lissu Wabunge kutoa nusu ya posho yao ya siku moja kuchangia matibabu ya Tundu Lissu Reviewed by Zero Degree on 9/08/2017 06:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.