Loading...

Wananchi waomba chakula kifutwe msibani

BAADHI ya wananchi wa Nzengo ya Amani ‘B’ Kata ya Nyihogo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani hapa, wameuomba uongozi wao wa mtaa kuifuta ratiba ya chakula msibani ili fedha za rambirambi zinazopatika zitumike kumfariji mfiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao wa Amani, Hawa Kasonso alisema kuwa anatamani kama uongozi ungepitisha azimio la watu kuchangia rambirambi msibani pasipo kula ili pesa ambayo ingetumika kwa chakula apewe mfiwa.

Mimi binafsi nakerwa na kitendo cha wananchi kuchangishana fedha nyingi msibani kisha fedha hizo zinaishia kununuliwa vyakula vinavyotumika katika msiba na kusahau kumtengea fungu kubwa mfiwa. Ushauri wangu tukichangia rambirambi tusile chakula ili fedha tumuachie mfiwa.

“Fedha nyingi ya rambirambi inatumika kimakosa, unakuta waombolezaji wanakule weee, halafu baada ya hapo."

wanasambaa na kumuacha mfiwa hana kitu, wakati huo atakuwa hafanyi kazi kwa siku kadhaa, sasa unategemea atakuwa anakulala nini na hapo wananzengo tunakuwa tumemsaidia nini?

Kama mfiwa ni mwanamke basi ndiyo anateseka hasa na watoto wake, lazima tubadilieshe mfumo wa kusaidiana kwenye misibasiyo kwenda kula na kuongeza umaskini. Utadhani huwa hatuli nyumbani labda kama kuna wengine wanasubiri misiba ili wale chakula kizuri, alisema Kasonso.

Source: GPL
Wananchi waomba chakula kifutwe msibani Wananchi waomba chakula kifutwe msibani Reviewed by Zero Degree on 9/12/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.