Loading...

Watu 44 mbaroni kwa kutaka kuwauwa wanawake wanne kwa kuwachoma moto


Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu 44 kwa tuhuma za kutaka kuwaua wanawake wanne kwa kuwachoma moto, kutokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa, amesema waliwakuta watuhumiwa hao wakiwasulubu wakinamama hao kwa bakora huku wakiwa wamewafunga kamba, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kwenda kuwaokoa.

Wanawake hao kwa sasa wapo katika hospitali ya rufaa ya Tabora walikokimbizwa na polisi ili kunusuru maisha yao kwa majeraha waliyoyapata.

Kamanda Mutafungwa amesema pamoja na watu hao kuna wengine ambao walikimbia, na jeshi la polisi wanaendelea kuwasaka ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua, na kusema kwamba taarifa zaidi zitatolewa.
Watu 44 mbaroni kwa kutaka kuwauwa wanawake wanne kwa kuwachoma moto Watu 44 mbaroni kwa kutaka kuwauwa wanawake wanne kwa kuwachoma moto Reviewed by Zero Degree on 9/19/2017 06:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.