Loading...

Watu 7 watiwa nguvuni kwa kupinga kikomo cha umri wa Rais nchini Uganda

Wanaharakati vijana wakiandamana kupinga kikomo cha umri wa rais
Takriban watu saba wametiwa nguvuni katika mji mkuu wa Uganda kampala , kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya muswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais.

Katiba ya sasa inasema kikomo cha umri wa urais ni miaka 75.

Mabadiliko ya katiba yatamruhusu rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021.


Umri halisi wa rais Museveni haufahamiki, lakini mtandao wa Wikipedia unasema ana umri wa miaka 73

Wanaharakati vijana wa kundi lijulikanalo kama-The Alternative, ambao waliandaa maandamano hayo, wanasema ofisi yao ilivamiwa jana na wanajeshi pamoja na polisi.

Wanadai laptop, compyuta pamoja na nyaraka nyingine za kampeni yao vilichukuliwa wakati wa uvamizi huo.
Watu 7 watiwa nguvuni kwa kupinga kikomo cha umri wa Rais nchini Uganda Watu 7 watiwa nguvuni kwa kupinga kikomo cha umri wa Rais nchini Uganda Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 03:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.