Loading...

Yanga yashindwa kufurukuta kwa Majimaji


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga, wamelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye dimba la Majimaji mjini Songea.

Majimaji ndio ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Peter Mapunda dakika ya 54. Mchezo uliendelea kwa Yanga kuongeza mashambulizi ikitafuta bao la kusawazisha lakin Majimaji walionekana kujilinda zaidi pamoja na kupoteza muda kwa kuanguka.

Yanga ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 79 kupitia kwa Donald Ngoma baada ya kupiga kichwa krosi ya Obrey Chirwa. Baada ya kusawazisha bao hilo Yanga iliendelea kulisakama lango la Majimaji lakini haikufanikiwa kuongeza bao na hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki kuwa 1-1.

Mtibwa Sugar imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC na kufikisha alama 9 ambazo zinaifanya ishike uongozi wa ligi katika raundi ya 3

Matokeo ya Mechi nyingine zilizocheza leo:
  • Stand United 0-1 Singida United
  • Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
  • Mtibwa 2-1 Mbao FC
  • Prisons 0-0 Ndanda FC
Yanga yashindwa kufurukuta kwa Majimaji Yanga yashindwa kufurukuta kwa Majimaji Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 09:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.