Loading...

Zaidi ya watu 50 mkoani Kigoma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujichukulia sheria mkononi


Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Songoye ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi katika kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika tukio ambalo pia wameteketeza kwa moto nyumba saba, magari mawili, pikipiki nne na mali za familia za watu sita ambao wanawatuhumu kufanya mauaji ya watu kijijini hapo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikina ili watajirike.

Uharibifu mkubwa wa mali mbalimbali umefanywa na wananchi hao ikiwa ni pamoja na ofisi ya mtendaji wa kijiji hicho huku mmoja ya watu walionusurika kuuawa pamoja na mashuhuda wa tukio hilo wakieleza namna mkasa huo ulivyotokea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Naibu Kamishna wa polisi Ferdinand Mtui amesema zaidi ya watu hamsini wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku Kaimu mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Marco Gaguti ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe akitoa wito kwa wananchi a kuacha kujichukulia sheria mkononi.




Zaidi ya watu 50 mkoani Kigoma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujichukulia sheria mkononi Zaidi ya watu 50 mkoani Kigoma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujichukulia sheria mkononi Reviewed by Zero Degree on 9/06/2017 12:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.