Loading...

Yusuph Manji avuliwa udiwani

Yusuf Manji akiwa na viongozi waandamizi na wanachama wa CCM
MFANYABIASHARA Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Hayo yamesemwa leo Jumatano na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo aliongeza kwamba amemwandikia Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kupanga uchaguzi mwingine.
Yusuph Manji avuliwa udiwani Yusuph Manji avuliwa udiwani Reviewed by Zero Degree on 9/06/2017 11:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.