Loading...

Zitto amjia juu Spika wa Bunge


Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitikia sana kama haoni jinsi heshima ya Bunge inavyoshuka.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge, Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni.

Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehangaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha.

"Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge anapigwa risasi mkutano wa bunge ukiendelea wabunge wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na spika Ndugai tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu anatuangusha angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya" alisema Zitto Kabwe.

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa Ndugai alitamani kufikia japo robo ya marehemu Sitta katika kuongoza shughuli za bunge lakini ameshindwa kufikia hata asilimia 10 ya Anna Makinda.

"Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 sasa hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge" alisema Zitto Kabwe.
Zitto amjia juu Spika wa Bunge Zitto amjia juu Spika wa Bunge Reviewed by Zero Degree on 9/12/2017 01:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.