Loading...

Alichosema Spika wa Bunge kuhusu Lazaro Nyalandu kujiuzulu

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na Lazaro Nyalandu 
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu na wala hiyo barua bado haijamfikia, amekiita kitendo alichokifanya ni umbea.

Kwa mujibu wa Taarifa ya GPL, Job Ndugai amesema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.

Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.
Alichosema Spika wa Bunge kuhusu Lazaro Nyalandu kujiuzulu Alichosema Spika wa Bunge kuhusu Lazaro Nyalandu kujiuzulu Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 02:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.